Kuhusu SokoKusini
SokoKusini ni nini?
SokoKusini ni jukwaa la mtandaoni linalolenga kuwaunganisha wanunuzi na wauzaji kwa njia rahisi. Jukwaa hili limekusudiwa kusaidia biashara ya mifugo, mazao ya kilimo na bidhaa nyingine.
Dhamira yetu
Dhamira yetu ni kurahisisha upatikanaji wa taarifa za bidhaa na kuwasaidia watu kutangaza na kutafuta bidhaa kwa urahisi kupitia simu au kompyuta.
Maono yetu
Tunataka kujenga soko la kidijitali linaloaminika, linalowafikia watu wengi na kusaidia kukuza biashara na fursa za kiuchumi katika jamii.
Karibu SokoKusini
Tunakukaribisha kutumia SokoKusini kutangaza bidhaa zako au kutafuta bidhaa unazohitaji. Tunajitahidi kuendelea kuboresha huduma yetu ili iwe rahisi na yenye manufaa kwa watumiaji.